Mwanamuziki kutoka nchini Marekani,Rick Ross akijisikia furahaa kuwaona
Watanzania wakiwa wamejitokeza kwa wingi kwa ajili ya kumshuhudia yeye
akikamua stejini.
Watu kibao wakiwa ndani ya viwanja vya lidaz club usiku huu.
Msanii wa miondoko ya rusha rohoo a.k.a Miduara,Shilole akijiachia
jukwaani vilivyo na madansa wake usiku huu mbele ya umati mkubwa
uliofika kwenye viwanja vya Lidaz Club,katika kuhitimisha kilele cha
tamasha la Serengeti Fiesta 2012.
Sehemu ya umati watu waliojitokeza kila kona jiji la Dar na kwingineko
kuwashuhudia wasanii mbalimbali wakitumbuiza kwenye jukwaa la tamasha la
Serengeti Fiesta 2012,akiwemo Mwanamuziki wa kimataifa kutoka nchini
Marekani,Rick Ross.
Wasanii wa kundi la Wanaume TMK,likiongozwa na Mh Themba sambamba na
Chege Chigunda wakilishambulia jukwaa vilivyo usiku huu kwenye tamasha
la Serengeti Fiesta 2012,linaloendelea hivi sasa katika viwanja vya
Lidaz Club,Kinondoni jijini Dar.uwanja wa Lidaz Club hapatoshi kabisa
usiku huu.
Nyomi la Watu ile balaa usiku huu.
Wasanii wa kikundi cha Makomando kutoka THT wakionesha umahiri wao wa kucheza jukwaa.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Dyana pichani akionesha mbwembewe zake
kabla ya kukamata kipaza sauti,mbele ya umati mkubwa uliojitokeza kwa
wingi usiku huu ndani ya viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni jijini Dar
Msaniii mahiri wa kizazi kipya,Barnaba Boya kiimba jukwaani huku Dyana na skwadi lake wakionesha mbwembwe zao kama kawa.
Mmoja wa wshindi wa shindano la Serengeti Supa Nyota 2012,Youk Killer
akishusha mistari yake nguvi usiku huu,huku shangwe na vigele vigele
vikiwa vimetawala.
Mashabiki wakishangweka usiku huu vilivyo.
Mmoja wa washindi wa shindano la Serengeti Supa Nyota 2012,Jo Maker akifloo jukwaani. .
Baadhi ya mashabiki wakijiachia vilivyo usiku huu ndani ya tamasha la Serengeti Fiesta 2012
Mmoja wa wshindi wa shindano la Serengeti Supa Nyota 2012,NeyLee akiimba jukwaani .
Baadhi ya wasanii kutoka nyumba ya vipaji THT wakiamsha amsha usiku huu
wakati tamasha la Serengeti Fiesta 2012 likiendelea huku mashabiki na
wapenzi wa tamasha hilo wakiendelea kumiminika usiku huu ndani ya
viwanja vya Lidaz Club,jijini Dar.
Mmoja wa wasanii chipukizi kutoka kwa THT,akiimba kwa hisia mbele ya
umati mkubwa wa watu (haupo pichani),uliojitokeza kushuhudia wasanii wa
hapa nyumbani na nje wakitumbuiza katika jukwaa moja usiku huu.
Mmoja wa wasanii chipukizi akinogesha jukwaa la Serengeti Fiesta 2012 usiku huu
The Wacko Jako wa bongo akifanya vitu vyake jukwaani usiku huu
Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar na vitongoji vyake wakiwa tayari ndani
ya viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni jijini Dar wakati wa
tamasha la Serengeti Fiesta likiendelea kurindima
No comments:
Post a Comment