Nguli wa Muziki wa Mwambao nchini na barani
Afrika Fatuma Binti Baraka maarufu kwa jina la Bi Kidude (zaidi ya miaka 90) amefariki
mchana huu.
Taarifa zilizoifikia Father Kidevu Blog zinasema
kuwa Bi Kidede amefariki majira ya saa 7 mchana wa leo nyumbani kwa ndugu yake
huku Bububu Kisiwani Zanzibar.
Aidha taarifa hizo zinaelezo kuwa Mipango yua
kuusafirisha mwili wa Marehemu inafanyika kutoka huko Bububu hadi Nyumbani
kwake Raha Leo.
Bi Kidude aliyekuwa akisumbuliwa na ugonjwa na
kulazwa mara kadhaa kifo chake kinaelezwa pia kuchangiwa zaidi na umri mkubwa.
Msiba huu ni mzto kuwahi kutokea kwa tasnia ya
muziki na Sanaa kwa ujumla kufuatia Mchango mkubwa wa Marehemu katika kukuza
muziki halisia wa mwambao.
Rais Jakaya Kikwete alimtunuku Bi Kidude Nishani
ya Uhuru wa Tanzania kwa mchango wake mkubwa alioutoa katika kipindi cha uhai
wake.
No comments:
Post a Comment
aminaplummer20@gmail.com