Footer 3

"I support Tanzania Asthma Foundation" DO YOU?

TANZANIA YACHUKUA NAFASI YA KUMI BORA NDANI YA LONDON FASHION WEEK...!!!

14. Wanamitindo wa Kitanzania kwenye London Fashion Week 2013. Anna Lukindo, Christine Mhando, Jacquiline Kibacha-pic by Urban Pulse 
Wanamitindo wa Kitanzania- Anna Lukindo, Christine Mhando na Jacqueline Kibacha Jumapili mchana wilaya ya Westminster jijini London ilikuwa na mashindano ya ubunifu na urembo katika maonyesho ya kimataifa ya London Fashion Week. Mashindano haya yalifanyika jumba la Somerset lililosimama imara kwenye upembe wa kaskazi ya mto Thames. 
 
Nje ya Jumba la Somerset- Samson Soboye, Jacqueline Kibacha, Mama Kallaghe, Anna Luks na Rose Kiondo-pic by Urban Pulse 
Nje ya Jumba la Somerset- Samson Soboye (Mpangaji wa maonyesho), Jacqueline Kibacha ("Heart 365"), Mama Balozi Joyce Kallaghe, Anna Lukindo ("Anna Luks") na Rose Kiondo (Mratibu wa maonyesho) Maonyesho ya London Fashion Week, bado yanaendelea jumba hili la Somerset toka tarehe 14 hadi tarehe 28. Wiki hizi mbili nzima zitakutanisha kila mtu anaye husika na biashara ya mavazi na urembo. Magwiji na mapapa wa mitindo, wabunifu, walimbwende, watafuta vipaji, wafanya biashara, wazalishaji mali ghafi na wamiliki viwanda. Wote hukutana katika maonyesho haya. Hapa si vipaji tu vinavyojionyesha, bali pia watu wa biashara.
Siku hii Tanzania ilikuwa moja ya nchi mbili tu za Kiafrika zilizochaguliwa na British Council na "London Fashion Week" kushiriki mashindano ya kutafuta vipaji chipukizi kwenye tasnia ya ubunifu wa mavazi na urembo. Watanzania Anna Lukindo, Jacqueline Kibacha na Christine Mhando ndio wasanii waliobeba bendera ya taifa letu na kutuwakilisha katika mashindano haya ya kimataifa yanayofanyika kila mwaka kwa zaidi ya miaka 27 sasa.
  Ubalozi umetoa Ukumbi wa Nyumba Ya Tanzania ulioko Bond Street ili wasanii hao waweze kuonyesha nguo na sanaa zao kwa juma zima kama sheria za London Fashion Week zinavyoamuru. Vile vile Bodi ya Utalii ya Tanzania imesaidia katika mchango wa mali ghafi zilizotumika katika shughuli hizi ili kuiuza Tanzania kimataifa. Anna Luks -pic by Urban Pulse 
Anna Luks Mshindi wa tukio alikua Estonia. Ingawa Tanzania haikuwa mshindi wa mwanzo- ilichaguliwa kati ya Kumi Bora jambo ambalo limetikisa nyoyo na vichwa vya waandaaji, wabunifu,wafanya biashara na watafuta vipaji vya kimataifa. Hii ni mara ya kwanza kwa taifa letu kushiriki katika shughuli na wote wameguswa na kupumbazwa na usanii wa hali ya juu ulioonyeshwa na wasanii watatu wa Kitanzania.  


Kwa hisani kubwa ya jestina-george

No comments:

Amina Design

"I support Tanzania Asthma Foundation" DO YOU?
"I support Tanzania Asthma Foundation" DO YOU? Amina Design
Amina Design