Flaviana Matata akikabidhi msaada wa maboya 500 kwa mwakilishi wa mkuu wa mkoa wa Mwanza, Elias Makori (kulia) ikiwa ni kumbukumbu ya miaka 16 ya ajali ya meli ya MV Bukoba, anayeshuhudia ni Meneja Masoko na Biashara wa Shirika la usafirishaji wa majini mkoani Mwanza la Marine Service, Kapten Obadia Nkongoki Igoma jijini Mwanza.
Flaviana Matata alishindwa kujizuia na kuangua kilio wakati wa ibaada ya kumbukumbu ya miaka 16 ya ajali ya meli ya MV Bukoba alipotembelea baadhi ya makaburi ya watu waliopoteza maisha katika ajali hiyo yaliyopo Igoma jijini Mwanza katika ajali hiyo Flaviana alimpoteza mama yake mzazi.

Flaviana na wageni wakiweka mashada kwenye makaburi ya waliofariki kwenye ajali hiyo Igoma Mwanza.

Waombolezaji wengine waliofiwa na ndugu zao wakiombea marehemu wa ajali hiyo