Kwanza napenda kumshukuru Mungu kwa kunikupa fursa hii ya kumuelezea mama yangu. kwa wanaomfahamu Bi. Khadija wanajua kuwa ndiye mkombozi wangu, lakini ni wajibu wangu kama mtoto kumuelezea kile kilicho moyoni mwangu.
Tangu napata akili namuona mama akituhangaikia ili tupate elimu na kuweza kuishi vyema. Hakuna aina yoyote ya kitafunio cha chai ambacho mama hajawahi kuuza.si maandazi, chapati, vitumbua nk. Familia yetu ilipoanza kuongezeka hakuna Mkoa unaotoa zao la kudumu, mama hajawai kwenda, Dagaa-Kigoma, Nyanya-Iringa au hata Magimbi Morogoro.
Hadi leo hii mama ni mshauri mkuu wa Amina Design Company Limited. Jitihada za mama ndio zimeifikisha kampuni hii hapa ilipo. Nimejifunza heshima, kujitegemea, kulea,kuongoza, kuwa mvumilivu katika ndoa, kujijenga kidini na jinsi ya kuishi na jamii. Ndio maana nimeweza kusimama kibiashara na kuwa mfano mzuri kwa watoto wangu. Mwaka jana nilipewa tunzo ya mama bora wa mwaka 2011 kutoka Almuntazir High school.
Siku ya ufunguzi wa Tawi letu kubwa la Amina Design lililopo Quality Centre Mall sikuona mgeni rasmi zaidi ya mama . Hakuna anayeweza kumpa cheo mama isipokua mimi ndiye ninayetambua kazi na tabu za mama yetu alizopata. Nilisikia raha sana mama alivyonifungulia milango ya baraka.
Nakupenda sana mama yangu, Mwenyezi Mungu akuondolee maradhi. Mwenyezi Mungu akuongeze umri tuzidi kukuona mama yetu. Amina.
My daughter Lakisha and son Abdulkarim
My son Seif Tyrese
Mariam Gospel Singer with her Baby girl
Miriam and owner of A design
Nancy Sumary with her daughter Zuri
Miriam Odemba with Baby Iris's
Begum and her son Zack from Belgium
Sarah Soso with her daughter Raqsa