Wanamitindo wa Kitanzania- Anna Lukindo, Christine Mhando na Jacqueline Kibacha
Jumapili mchana wilaya ya Westminster jijini London ilikuwa na
mashindano ya ubunifu na urembo katika maonyesho ya kimataifa ya London
Fashion Week. Mashindano haya yalifanyika jumba la Somerset
lililosimama imara kwenye upembe wa kaskazi ya mto Thames.
Nje
ya Jumba la Somerset- Samson Soboye (Mpangaji wa maonyesho), Jacqueline
Kibacha ("Heart 365"), Mama Balozi Joyce Kallaghe, Anna Lukindo ("Anna
Luks") na Rose Kiondo (Mratibu wa maonyesho)
Maonyesho ya London Fashion Week, bado yanaendelea jumba hili la Somerset toka
tarehe 14 hadi tarehe 28. Wiki hizi mbili nzima zitakutanisha kila mtu
anaye husika na biashara ya mavazi na urembo. Magwiji na mapapa wa
mitindo, wabunifu, walimbwende, watafuta vipaji, wafanya biashara,
wazalishaji mali ghafi na wamiliki viwanda. Wote hukutana katika
maonyesho haya. Hapa si vipaji tu vinavyojionyesha, bali pia watu wa
biashara.
Siku
hii Tanzania ilikuwa moja ya nchi mbili tu za Kiafrika zilizochaguliwa
na British Council na "London Fashion Week" kushiriki mashindano ya
kutafuta vipaji chipukizi kwenye tasnia ya ubunifu wa mavazi na urembo.
Watanzania Anna Lukindo, Jacqueline Kibacha na Christine Mhando
ndio wasanii waliobeba bendera ya taifa letu na kutuwakilisha katika
mashindano haya ya kimataifa yanayofanyika kila mwaka kwa zaidi ya miaka
27 sasa.
Ubalozi umetoa Ukumbi wa Nyumba Ya Tanzania
ulioko Bond Street ili wasanii hao waweze kuonyesha
nguo na sanaa zao kwa juma zima kama sheria za London Fashion Week
zinavyoamuru. Vile vile Bodi ya Utalii ya Tanzania imesaidia katika
mchango wa mali ghafi zilizotumika katika shughuli hizi ili kuiuza
Tanzania kimataifa.
Anna Luks
Mshindi wa tukio alikua Estonia. Ingawa Tanzania haikuwa mshindi wa mwanzo- ilichaguliwa kati ya Kumi Bora
jambo ambalo limetikisa nyoyo na vichwa vya waandaaji,
wabunifu,wafanya biashara na watafuta vipaji vya kimataifa. Hii ni mara
ya kwanza kwa taifa letu kushiriki katika shughuli na wote wameguswa na
kupumbazwa na usanii wa hali ya juu ulioonyeshwa na wasanii watatu wa
Kitanzania.
Kwa hisani kubwa ya jestina-george
No comments:
Post a Comment
aminaplummer20@gmail.com