Pages

SHOPPING YA WEMA SEPETU KUFURU


HII ni safu mpya ambayo inamhusu staa wa fani yoyote, mwanamke au mwanaume ambaye atakuwa amenaswa akinunua bidhaa za matumizi yake. Wiki hii tunaanza kuangalia ‘shopping’ ya staa wa filamu za Kibongo, Wema Isaac Sepetu ambayo kiukweli ilikuwa kufuru.

Mrembo huyo alinaswa hivi karibuni akifanya manunuzi ya nguo tu, zenye thamani ya Sh. milioni 4.3 katika duka la Amina Designer lililopo ndani ya Jengo la Quality Centre jijini Dar.
“Ni utamaduni wa kawaida kwangu kufanya shopping mara kwa mara. Sioni uchungu wa kutoa fedha, labda ni kwa sababu natumia kadi kulipia, ningekuwa natoa kwenye pochi na kuhesabu kumpa muuzaji, nisingeweza kufanya hivyo, fedha nyingi kama ile ukiishika mkononi na kulipa kununua nguo roho inauma,” alisema Wema.

 
 

 
 
Habari na globalpublishers

No comments:

Post a Comment

aminaplummer20@gmail.com